Friday, March 24, 2017

SIKILIZA WIMBO TOKA BESTSONG GROUP TOKA GOMA NCHINI DRC.




Kundi hili la BestSong ni kundi linalopatikana katika mji wa Goma nchini DRC.
Kundi hili linapatikana katika anisa la Waadventista wasabato Himbi lililopo Goma DRC. Kundi hili lilianza mnamo mwaka 2012 likiundwa na vijana wapatao tisa (9) wakiwa na lengo la kuhubiri injili nchini Congo na ulimwenguni kote kupitia uimbaji.

Kundi hili Wamefanikiwa kutoa albam yao ya kwanza mwaka huu 2017 ikiwa na nyimbo Saba, ambazo zimeimbwa kwa Acapella na kwa kutumia ala za muziki.
kwa sasa kundi hili lina jumla ya waimbaji 7,  

  • Michael LUVATSUNGANA,  
  • Josue NKIZINKIKO
  •  Amini SINIGENGA
  •  Jilson MBAMBA,
  •  Daniel MUKUMBA,  
  • Philemon HABIMANA,  
  • James MIYISA.

Vijana hawa wako chini ya uangalizi wa viongozi toka kanisa la Himbi nao ni 
  •  Olivier LYAKE president,
  •  Esther BAABO vice president, 
  • Adeline KASONGO Mshauri, 
  • Samy WAVO Mshauri


Friday, March 10, 2017

PICHA 3:MIRIAM CHIRWA AKIWA NCHINI KENYA

ABG -ONLINETV


Picha tatu zikionyesha matukio mbalimbali za muimbaji Wa nyimbo za injili MIRIAM CHIRWA akiwa nchini kenya.






Akiwa nchini Kenya alipata fursa ya kufanya
 Mahojiano na Television ya K24TV ya Kenya.

#Kwa habari mbalimbali Like page yetu @abgonlinetv

Contacts:
+255659570630
+255659445425

Friday, March 3, 2017

UBATIZO MKUBWA WAFANYIKA TANZANIA.

ABG ONLINETV.


Ubatizo mkubwa wa kihistoria umefanyika leo Tar 03.03.2017,nchini Tanzania jijini Mwanza katika Hotel yenye hadhi ya Kimataifa ijulikanayo kwa jina la VICTORIA PALACE HOTEL, ambapo watu zaidi ya 800 wamebatizwa.

Ubatizo huo nimatokeo ya mahubiri makubwa ya julikanayo kama USHINDI HATIMAYE yanayoendelea jijini mwanza ambayo yanaendeshwa na kanisa la waadventista wasabato kupitia chama cha wanataaluma na wajasiriamali (ATAPE), ambapo mafundisho mbalimbali ya neno la MUNGU yamekua yamekua yakitolewa.



Katika mahubiri hayo mpaka sasa watu zaidi ya 5,000 wamebatizwa kwa maji mengi na wengine wanaendelea kubatizwa, sambamba na hilo wachungaji watatu wa madhehebu tofauti wamemkiri yesu na kubatizwa kwa maji Mengi na kujiunga na kanisa la waadventistwa wasabato ulimwenguni.

Mahubiri hayo yanatarajiwa kuhitimishwa leo katika kanisa la waadventista wasabato MABATINI mwanza.

 



''MWANZA 2017---- USHINDI HATIMAYE''

 Lile page yetu kwa habari mbalimbali@AbgOnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

Tuesday, February 28, 2017

Nokia 3310 yazinduliwa upya katika mfumo na mwonekano mpya

Kampuni ya simu ya Nokia imezindua upya simu aina ya nokia 3310 ambayo kwa sasa inakuja na muonekano mpya ambao unavutia zaidi kioo cha rangi yebye kuweza kuonekana vizuri kwa watumiaji wake.




Aidha simu hii ina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa mwezi mmoja bila kuchaji, betri yake imeingezewa ubora ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wake ambao mara nyingi watu hutamani kukaa na simu inayodumu na chaji kwa muda mrefu.

Pia simu hii imekuja na mchezo wa nyoka au snake xenzia game ambo ni maarufu kwa sinu nyingi za nokia.
Simu hii ina ukubwa wa kioo cha 2.4inch
Ina teknolojia ya 2G kwa ajili ya mtandao
Ina camera ya 2MP
Teknolojia ya bluetooth 3.0
Ina radio ya FM
Pia ina weza kucheza miziki katika mfumo wa MP3
Ina uwezo wa kufihadhi data mpaka 16MB
Na pia inasehemu ya kuweka memory card mpaka 32GB

Simu hii itapatikana kwa gharama ya Euro49 zaidi ya Tsh. 120,000/-


Like page yetu kwa habari zaidi @abgonlineTv
Abg OnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

MAFUA YA NGURUWE YASHAMBULIA MAGHARIBI MWA TANZANIA


ABG ONLINETV.


Mlipuko wa homa ya mafua ya nguruwe walikumba eneo la magharibi mwa Tanzania

Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe umeikumba wilaya ya Kalambo mkoa Rukwa kusini magharibi mwa Tanzania, na kusababisha vifo vya nguruwe karibu 200.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Bibi Julieth Binyura amesema serikali imepiga marufuku biashara ya nyama hiyo, na usafirishaji wa nguruwe hai ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Bibi Binyura pia amesema wanavijiji wa wilaya hiyo wamearifiwa kuhusu ugonjwa huo. Ofisa mifugo wa Wilaya hiyo Bw Wilbrod Kansapa amesema nguruwe wanaoonekana wakirandaranda wanakamatwa.

Ufugaji wa nguruwe unaendelea kuongezeka katika maeneo ya magharibi mwa Tanzania, kutokana na mahitaji makubwa kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam.

CHANZO: CRI KISWAHILI

 
 UGONJWA WA MAFUA YA NGURUWE
  • Ni aina mpya ya homa inayosababishwa na virusi ambavyo ni rahisi kuambukizwa, na rahisi kuambukiza watu wengine.
  • Wagonjwa wa kwanza waliambukizwa mnamo April 2009 na ugonjwa huo umeenea upesi katika nchi nyingi duniani. 
DALILI ZAKE
Kama wewe au ndugu yako ana homa au ongezeko la joto la mwili
(zaidi ya 38°C / 100.4°F) na unaweza kuwa na mafua ya nguruwe
kama una dalili mbili au zaidi zifuatazo:
  • uchovu ambao sio wa kawaida
  • kuumwa kichwa
  • kuwa na mafua
  • maumivu ya koo
  • kushindwa kupumua na kukohoa
  • kukosa hamu ya kula
  • maumivu ya misuli
  • kuharisha na kutapika
JINSI UNAVYOSAMBAZWA  
Watu wenye homa ya mafua ya nguruwe, wanasambaza virusi kwa njia ya kikohozi au chafya, na watu wengine wanavuta hewa yenye virusi. Virusi vinaweza kuishi katika mikono na sehemu zingine kwa zaidi ya masaa 24.
JINSI YA KUJIKINGA WEWE NA FAMILIA YAKO.
  1. Zuia mdomo na pua kwa kitambaa kisafi au karatasi laini wakati unapokohoa au kupiga chafya. 
  2. Tupa kitambaa kwenye pipa la taka baada ya kukitumia.
  3. Osha mikono yako na sabuni na maji au na sabuni ya mikono yenye dawa ya kuulia virusi mara kwa mara na safisha sehemu za juu kila mara ili kuua virusi.
  4. Wajue marafiki watakaokusaidia. Wanaweza kuwa jirani zako, marafiki au ndugu wanaoweza kukusaidia wakati unapoumwa. Kwa mfano, wanaweza kwenda kukuchukulia dawa na chakula.
  5.  Kama wewe ni muomba hifadhi na una homa ya mafua ya nguruwe, wewe au rafiki yako ni lazima kuwasiliana na mfanyakazi wa Idara ya Uhamiaji (United Kingdom Border Agency) anayesimamia kesi yako ili wafanye mpango mwingine wakuchukua pesa zako za ruzuku, ili usiwe na haja ya kutoka mahali unapoishi. Ni lazima uwasiliane na msimamizi wa kesi yako au sehemu unayoripoti ili wafanye mipango mipya ya kuripoti.
  6. Kama ni mjamzito, endelea kufanya shughuli zako za kawaida, kama vile kwenda madukani, kutumia usafiri wa umma na kushiriki katika mikusanyiko ya kifamilia. Lakini ni vizuri kama hutawatembelea ndugu na marafiki wenye dalili za homa ya nguruwe. Kama unajua kwamba kuna wagonjwa wengi wanaoishi karibu na nyumbani kwako, ni vizuri kuepuka na mikusanyiko ya umati ya watu

Like page yetu kwa habari zaidi @abgonlineTv
Abg OnlineTv
+255659570630
+255659445425
+255714007330

Monday, February 27, 2017

MIRIAM CHIRWA ABATIZWA KWA MAJI MENGI.


ABG ONLINETV

Muimbaji wa nyimbo za injili MIRIAM CHIRWA amempokea yesu kwanjia ya  ubatizo wa maji Mengi, katika ubatizo uliofanyika jumamosi Tar 25/02/2017, katika kanisa la waadventista wa sabato Temeke jijini Dar es Salam.


Ambapo aliambatana na watu zaidi ya 50 waliojitoa kubatizwa kutokana na Mkutano mkubwa  wa injili unaoendelea jijini Mwanza ujulikanao kama  USHINDI HATIMAYE unaosimamiwa na kanisa la waadventista wa sabato kupitia  chama cha wanataaluma na wajasiriamali (ATAPE),




 Mahubiri hayo yanarushwa mubashara kutoka katika kanisa la waadventista wasabato Mabatini Mwanza kupiti vituo mbalimbali vya Television na Radio ambavyo ni Morning star Tv na Radio, Star Religion .

Endelea kufatilia mahubiri hayo na kwa hakika utabarikiwa




abg -Online Tv
+255659445425
+255659570630
+255714007330

Sunday, February 5, 2017

MUIMBAJI WA AMBASSADORS YOMBO AFUNGA NDOA RASMI.


 Na. ABG -ONLINE TV
Muimbaji wa Ambassadors Yombo SDA,  Lilian Daniel amefunga ndoa rasmi na Ndugu Elio Richard , Ndoa hiyo imefungwa leo Tar 5/02/2017  katika kanisa la waadventista wasabato GANGILONGA IRINGA.

ABG online tv tunawatakia mafanikio katika safari hiyo ya maisha na Mungu wa mbinguni awabariki sana.
   

Mr & Mrs Elio katikati pamoja na Mates na Matrons.
Mr & Mrs Elio Richard katika pozi
Mdogo wa bibi arusi Amos daniel (kushoto) na Salome kepha (kulia,)


Bibi arusi na rafiki na mwana chama mwenza wa Ambassadors yombo
 Contacts:
ABG - ONLINE TV
+ 255659570630
 +255659445425
+255714007330